Feasts

 

SIKUKUU ZA BWANA.

 

Pasaka ya Bwana

Kanisa la Mungu Kenya, linafuraha kukualika kwenye sherehe maalum ya Bwana Mungu wetu. Sherehe hii ilitangazwa rasmi naye Bwana wetu, katika kitabu cha walawi 23. 4, Sikukuu za Bwana ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayapigia mbiu kwa nyakati zake. Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni pasaka ya Bwana.

Tarehe hiyo inaingiliana na tarehe 26 jioni, kwanzia tarehe 27. mwezi wa tatu kalenda ya Gregori inayo tumika kwa sasa.

Sikukuu ya Mikate isiyotiwa chachu

Baada ya Pasaka ya Bwana, tutasherekea sikukuu ya mikate isiyo tiwa chachu. Walawi 23:6 Na siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa Bwana ya mkate usiotiwa chachu; mtaila mikate isiyochachwa muda wa siku saba.

Fungu la 7. Siku ya kwanza mtakua na kusanyiko takatifu msifanye kazi yo yote ya utumishi.

Hiyo itakua tarehe 27 jioni, kuanzia tarehe 28, mwezi wa tatu.

Karibuni nyote.

Tuzidi kuombea Janga la Virusi vinavyo sababisha Korona.

Ime bainika kwamba, kumeibuka awamu ya tatu ya kuenea virusi hivi. na awamu hii vina makali kabisa.

Tuweke hoja zetu kwa Bwana, tumtumai nyakati zote, tunapo fuata masharti ambayo yame wekwa na wataalamu wa afya duniani. imetupasa kuyaheshimu mamlaka yalioko.

Tuwaombee waliopoteza wapendwa wao.